Jana tarehe 8 Mei 2025 Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi ikiongozwa na Mhe:Kuruthum Issa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa imefanya ziara maalumu ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Pangaboi uliopo kata ya Nachunyu wenye thamani ya shilingi 500,000, 000/= , Mradi wa shule ya Sekondari ya Wavulana kanda ya kusini uliopo katika kata ya Kiwalala wenye thamani ya Shilingi 4,100,000,000/= lakini pia Mradi wa shule ya Msingi Mtakuja wenye thamani ya shilingi 331,000,000 na Mradi wa Shule ya Sekondari Mtakuja wenye thamani ya shillingi 560,552,827.
Akiongea na wajumbe pamoja na Wananchi katika ziara hiyo Mhe: Kuruthum amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtama na timu nzima ya wataalamu kwa kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa kuzingatia ubora na ilani ya Chama cha Mapinduzi lakini pia Mhe: Kuruthum amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawahimiza watoto wao kusoma kwa bidii ili kuyatumia majengo yote ya shule za kisasa zinazojengwa ndani ya Halmashauri ya Mtama.
Aidha Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Lindi Mhe: Athumani Hongonyoko amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT: Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika Mkoa wa Lindi hasa katika sekta ya Afya, Elimu na Maji.
Kwa upande wa Bwn: Patrick Magalinja Katibu wa Siasa na Uwenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM amewasihi Wananchi wote wa Halmashauri ya Mtama kuhakikisha wanajitokeza kufanya maboresho katika Daftari la Kudumu la Mpiga kura kwa awamu ya pili ili kupata haki ya msingi ya kupiga kura, Zoezi hilo la uboreshaji wa taarifa linatarajia kuanza rasmi tarehe 16 hadi tarehe 22 Mei mwaka huu.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.