Wahudumu wa afya ngazi ya jamii (CHW) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Jana tarehe 02 Septemba 2025 wamekabidhiwa vifaa mbalimbali vya kazi kutoka Wizara ya Afya, Vifaa hivyo ni pamoja na Vitabu vya Mtaa no 3, mabegi ya mgongoni, Tisheti, BP mashine, Rain boot nakadhalika, Tukio hilo limefanyika katika kituo cha afya Mtama kilichopo kata ya Mtama.
Vifaa hivyo vimetolewa kwa wahudumu waliomaliza mafunzo yao katika vyuo vitatu vya afya vinavyotoa mafunzo kwa kada hiyo: Masasi Cohasi, Nachingwea SON, na Mtwara COHAS. Lengo la utoaji wa vifaa hivyo ni kuwawezesha wahudumu hao kutekeleza majukumu yao ya kutoa elimu ya afya kwa jamii kwa ufanisi zaidi, hususan katika maeneo ya pembezoni.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Ndugu Edwin Ngonyani, Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama aliyekabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, aliwataka wahudumu hao kutumia vifaa walivyopokea kwa malengo yaliyokusudiwa. Alisisitiza umuhimu wa kujituma na kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu na huduma za afya majumbani, kwa kuzingatia kauli mbiu ya programu hiyo: "Nyumba kwa Nyumba, Hatuachi Mtu"
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.