Katibu Tawala Wilaya ya Lindi Ndugu Hudwaifa Rashidi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi leo tarehe 02 Septemba 2025 ameongoza kikao maalum cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe kwa Robo ya nne kwa ngazi ya Wilaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, kikao hiko kimefanyika katika ukumbi mdogo wa Mikutano uliopo Halmashauri ya Mtama huku lengo la kikao hiko ikiwa ni kupokea, kujadili na kutathmini hali ya lishe katika Halmashauri ya Mtama.
Akitoa Tathmini ya Lishe kwa wajumbe wa kikao hiko Ndugu Gozbert Henerico Mratibu wa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Mtama amewapongeza watendaji wa kata pamoja na wataalam kwa kuhakikisha kuwa shule zote zilizopo Halmashauri ya Mtama zinatoa huduma ya upatikanaji wa chakula shuleni kwa asilimia 97 hali iliyopelekea kufanya vizuri katika kiashiria hiko cha lishe.
Naye Ndugu Hudhwaifa Rashidi Mwenyekiti wa kikao hiko kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi amesisitiza utoaji wa hamasa za mara kwa mara ili kuhakikisha wananchi wapate kile ambacho Serikali imekusudia kutoa kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa lishe bora kwa jamii lakini pia amewataka wataalam wote kwa ujumla kushirikiana kila mmoja kwa nafasi yake ili kuhakikisha lishe inapatikana kwa ufanisi shuleni na nyumbani.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.