Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. George Mbilinyi Machi 14, 2022 ametembelea Mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Chiponda na kusisiza uwajibikaji wa hali ya juu ili kufikia lengo la kukamilika kwa mradi huo.
Agizo hilo limekuja mara baada ya kuona hali ya ujenzi huo ukisuasua ambapo aliendelea kuwasisitiza wajumbe wa kamati kuhakikisha wanatekeleza mradi huo kwa uzalendo, ushirikishwaji pamoja na kuhakikisha wanatumia maarifa katika kupunguza gharama za matumizi ya fedha ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wananchi kujitolea.
Aidha Ndg. Mbilinyi akiwa na wataalamu kutoka Hakmashauri alitembelea kituo shikizi Ntemanje kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi.
Box 328 Lindi
Postal Address: 328 Lindi Dc
Telephone: 0222061
Mobile:
Email: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.