Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe: Victoria Mwanziva ameitaka kamati ya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kuhakikisha inaongeza jitihada katika kuhamasisha wanaume Kushiriki afua za Lishe, Ameyasema hayo Leo tarehe 29 Aprili 2025 katika kikao maalumu Cha Tathmini ya Lishe kwa robo ya tatu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Halmashauri ya Mtama.
DC Mwanziva aliongeza kuwa uhamasishaji huo ni pamoja na kuandaa siku maalumu ya kutoa elimu Kwa akina baba kuhusu umuhimu wa Lishe bora Kwa watoto, watu wazima na wajawazito, hamasa hiyo itaenda kuongeza ushiriki wa wanaume katika mambo mbalimbali yanayohusu Lishe bora kwani ushiriki wao ni hafifu kwasababu ya kutokuwa na Elimu ya kutosha.
Akiongea na wajumbe wa kikao hiko Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndugu Anderson Msumba amewataka watendaji wa kata na vijiji kushirikiana na kamati ya Afya ili kuhakikisha afua za Lishe zinatekelezwa katika ngaza za kata na vijiji ikiwa ni pamoja na utoaji wa vyakula Lishe mashuleni na kuendeleza mashamba ya matunda na mbogamboga ili kurahisisha upatikanaji wa Lishe bora mashuleni.
Aidha Mratibu wa Lishe Halmashauri ya Mtama Ndugu Gozbert Henerico amewasisitiza wajumbe wa kikao hiko kutoa elimu ya kutosha Kwa wajawazito kuhudhuria kliniki kwa wakati ili kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga lakini pia kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa na kilo pungufu.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.